8 Aprili 2015 - 11:57
New York Times: Netanyahu apatwa na maluweluwe

Gazeti la New York Times katika kichwa cha habari cha Makala inayohusu makubaliano ya nyuklia baina ya Iran na nchi zenye nguvu duniani imeandika kuwa Benjamin Netanyahu waziri mkuu wa utawala wa kizayuni amepatwa na maluelue kuhusu makaubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran na nchi zeneye nguvu duniani

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: gazeti hilo la Mraekani limeandika: hakuna mazungumzo yoyote yasiowezekana kufikiwa makubaliano, ama waziri mkuu wa Israel alipatwa na maluweluwe nakufikiri kuwa anaweza kuweka masharti yake katika mazungumzo hayo baina ya Iran na kikundi cha 5+1.
Waziri mkuu huyo alikuwa anafikiri kuwa kupinga kwake makubaliano hayo kutasababishwa kutofikia muafaka  katika mpango wa nyuklia wa Iran na mataifa yalio na nguvu duniani.
Kwamujibu wa ripoti ya gazeti hilo la kimarekani utawala haramu wa kizayuni siku ya jumatatu umetoa masharti mapya ili kufika katika kile alichokidai kuwa kuongezwa kwa masharti hayo kutapelekea kupata makubaliano mazuri katika muafaka huo.
Masharti hayo yliotolewa na Netanyahu kwaujumla hayaiingii akilini, hivyo kwakuwa utawala wa kizayuni watilia mkazo masharti hayo yawepo katika makubaliano hayo, ama bishaka sikwamba makubaliano mazuri hayata patikana bali kamwe hakutapatikana makubaliano.
New York Times limeandika kuwa (Netanyahu) anafikiri kuwa yeyepekee ndiye anaeweza kukwamisha mwenendo wa makubaliano hayo, haliyakuwa miezi 18 mazungumzo yakutafuta muafaka hayakufanyika baina ya Iran na Marekani tu, bali nchi nyingi zikopamoja kutafuta muafaka wa utatuzi huo wa mazungumzo ya kisiasa ambapo Uingereza, Ufaransa, Ujeruman, Urusi na China zote zilishiriki katika mazungumzo hayo.
Anachokitaka waziri huyo wa kizayu nikuonyesha kuwa yeye ndeye mwenye akili zaidi kuliko wengine, kwani siku ya Jumapili alipokuwa akifanya maojiano katika Televishen ya NBC News miungoni mwa maelizo yake anasema: lengo langu sikuvuruga makubaliano bali najitahidi ili kusawazisha makubaliano mabaya yaliotokea.
Gazeti hilo limebainisha kuwa: hakuna mazungumzo yoyote yasiokuwa na uwezekano wa kufikia mauafaka, suala muhimu nikwamba imefahamika kuwa mpango wa nyuklia wa Iran nikwaajili ya matumizi ya amani katika maendeleo ya Iran.